Majukwaa | Majadiliano
Tupendekeze; tutoe maoni, tuulize kwa ajili ya kuondoa, kuhuisha; utunzi, urekebishaji na utekelezaji wa sera, sheria na kanuni; na tutoe tutathimini na mbinu za utekelezaji wenye tija kwa wadau wa Ushirika.
Tujadili namna bora ya miundo ya bodi, secretariet ambayo itakuwa na tija; katika kuhakikisha maslahi ya vyama vya ushirika na wanachama yanapatikana, ya uhakika na yanakuwa endelevu. Kuangalia mifumo ya usimamizi, kupima mafanikio na kupata mafanikio, kupunguza hasara na kutumia rasimali fedha, watu, miundombibu, habari vizuri n.k.
Tuangalie kwa undani namna habari na rasilimali (fedha,vitu, habari, fomu…) zinavyo badilishana mikono kwenye sekta nzima, utunzaji wake, namna rahisi ya kuipata inavyohitajika, ulinzi wake na kujua nani ana mamlaka gani? na mipaka yake ni wapi? Wapi kuna madhaifu na yarekebishwe ili kuwe na mnyororo ambayo unaendesha sekta ya Ushirika kilaini sana.
Nini matarajio yetu; nini tunataka mifumo ifanye? nini hatutaki mifumo ifanye? nini ni muhimu, nini sio muhimu sana, elimu gani tupate, ni mfumo gani wa ufikishaji (delivery) ni wenye tija; tuende vipi? changamoto za mifumo ni nini? je watu wetu? je mambo ya umeme, ofisi, usalama etc. Kwa mitazamo yetu, tunataka hali iwe vipi?

Excellence in Ushirika
We Intend to ensure our Ushirika model and value delivery, become the best and center of excellence for all Africa and Asian Cooperative to come, learn and from it.